Selcom Pesa Yashirikiana na Showmax kuwezesha Malipo bila makato kupitia kadi ya kidijitali Ya Selcom Pesa.
Ushirikiano wa kipekee kati ya Selcom Pesa na Showmax unahakikisha kwamba watumiaji sasa wanaweza kufurahia burudani ya kiwango cha juu kupitia Showmax kwa kutumia Kadi ya Kidijitali ya Selcom pesa ikiwapa uzoefu wa malipo wa haraka, salama bila gharama yoyote.
Hivi ndivyo unavyoweza kujisajili:
Pakua aplikesheni yako ya Showmax kwenye App Store au play store.
Pakua App ya Selcom Pesa
Jisajili mwenyewe kwa dakika chache tu, inayohitajika ni NIDA namba yako tu
Tengeneza akaunti yako
Baada ya kukamilisha usajili, utapata namba yako ya kadi ya kidijitali ya Selcom pesa ambayo itakuwezesha kufanya malipo ya Showmax bila makato.
Nakili namba yako ya selcom pesa ya kadi yako ya kidigitali.(Virtual card) kisha ukamilishe malipo kwenye ukurasa wa malipo kwenye tovuti ya Showmax.
Showmax inaendelea kutoa sinema, mfululizo, michezo ya moja kwa moja, na maudhui ya ndani kwa watazamaji wake. Hata hivyo, changamoto za malipo mara nyingi zimekuwa kikwazo kwa watumiaji. Ushirikiano huu mpya unalenga kuondoa vikwazo hivyo, kuhakikisha Watanzania wanapata huduma na burudani ya kiwango cha juu bila makato yoyote.
Kwa kuunganisha teknolojia ya kadi ya kidijitali ya Selcom Pesa na Showmax, wateja sasa wanaweza kujisajili kwa urahisi bila wasiwasi kuhusu malipo ya ziada wateja watalipia huduma ya Showmax hakuna ada au gharama za ziada. Ushirikiano huu unatoa suluhisho la malipo ya kidijitali kwa gharama nafuu.