Akaunti kamili ya benki, mkononi kidijitali.
Hifadhi, tuma, lipa, kopa na tumia kadi yako yote kupitia simu yako.
Makato yapo chini hadi 60% ukilinganisha na benki au pochi yako ya simu
Ya kwanza ya aina yake nchini Tanzania
Mabando ya miamala
Kwa nini ulipe kwa kila muamala wakati unaweza kujiwekea kifurushi? Ukiwa na Selcom Pesa Transaction Bundles, unapata miamala mingi kwa ada moja nafuu, hivyo kupata thamani zaidi na udhibiti mkubwa wa matumizi yako ya kila siku ya kibenki.
BUKU KWA SIKU – TZS 1,000
Miamala 7
Inatumika kwa saa 24
Hadi TZS 1,000,000
Nzuri kwa kutuma pesa na kulipia bili kwa haraka
WIKI BOOST – TZS 2,500
Miamala 35
Inatumika kwa siku 7
Hadi TZS 5,000,000
Nzuri kwa kutuma pesa, kulipia bili na kufanya manunuzi
HELLO MWEZI – TZS 10,500
Miamala 150
Inatumika kwa siku 30
Hadi TZS 50,000,000
Kifurushi kimoja. Urahisi wa mwezi mzima.
Akaunti ya benki iliyo kwenye simu yako. Selcom Pesa huwapa Watanzania sehemu moja ya kuhifadhi pesa, kutuma na kupokea, kutumia na kukuza fedha zao, ikiwa na ulinzi na usalama wa benki yenye leseni, si salio la mtandao wa simu tu.
Tuma Pesa
Tuma pesa kwenda benki, mtandao wa simu na kwa wapokeaji wengi kupitia app moja.
Wakati mwingine maisha hayangoji mshahara. Wateja wanaokidhi vigezo vya Selcom Pesa wanaweza kupata mikopo ya kidijitali moja kwa moja kupitia app.
Kopa
Lipa
Lipa kwa QR kwa wafanyabiashara kote nchini. Lipa bili za GePG, muda wa maongezi, LUKU, usajili wa TV, usafiri, michezo ya kubashiri na mengine mengi.
Tuma Kimataifa
Unganisha zaidi ya Tanzania. Tuma pesa kwenda China, DRC, India, Kenya, Msumbiji, Rwanda, Afrika Kusini, Uturuki, Uganda, UAE, Zambia na Zimbabwe.
Tumia kadi
Kadi za Mastercard Debit na Prepaid.
Chagua kadi ya kidijitali au ya plastiki, inayokubalika mtandaoni, kwenye ATM na popote duniani.
Lipa Later
Tumia sasa, lipa baadaye kwa wafanyabiashara waliochaguliwa, wakiwemo Puma Energy, Lake Energies, KFC, Pizza Hut na wengine.
Hakuna foleni. Hakuna makaratasi.
Fungua akaunti Selcom Pesa. Dakika 3 tu!
01 Download the app
Download the Selcom Pesa App from the App Store or Google Play.
02 Enter your details
Enter your valid mobile number, NIDA number when prompted or use your passport.
03 Verify your identity
Biometric verification using your fingerprint and facial biometrics.
04 Setup your account
Create your secure login credentials and complete the registration process.
Weka pesa. Anza kufanya miamala.
Kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Selcom Pesa ni rahisi.
-
upitia USSD au app ya mtandao wako wa simu:
Nenda kwenye Tuma Pesa kwenda Benki.
Chagua Selcom Microfinance Bank.
Weka namba ya akaunti yako ya Selcom Pesa au namba ya simu iliyosajiliwa na akaunti yako ya Selcom Pesa.
Weka kiasi cha pesa unachotaka kuongeza.
Weka PIN yako kuthibitisha muamala.
-
Unaweza kuhamisha pesa kutoka benki ya ndani moja kwa moja kwenda kwenye akaunti yako ya Selcom Pesa.
Fungua app ya benki yako au tumia huduma yake ya USSD.
Chagua Tuma Pesa kwenda Benki.
Chagua Selcom Microfinance Bank.
Weka namba ya akaunti yako ya Selcom Pesa au namba ya simu iliyosajiliwa.
Weka kiasi cha pesa.
Thibitisha muamala kwa kutumia PIN yako.
-
Tembelea Selcom Huduma Wakala aliye karibu nawe.
Mkabidhi wakala pesa taslimu unayotaka kuweka.
Mpe taarifa za akaunti yako ya Selcom Pesa, namba ya simu iliyosajiliwa au namba ya kadi.
Utapokea SMS ya uthibitisho mara pesa zitakapowekwa kwenye akaunti yako.
-
Tembelea Selcom Xperience Center iliyo karibu nawe.
Toa pesa taslimu unayotaka kuweka.
Wasilisha taarifa za akaunti yako ya Selcom Pesa, namba ya simu iliyosajiliwa au namba ya kadi.
Utapokea SMS ya uthibitisho mara pesa zitakapowekwa kwenye akaunti yako.
Selcom Zaidi. Panda daraja!
Kadri unavyotumia Selcom Pesa, ndivyo unavyofungua fursa zaidi!
Kutana na Selcom Zaidi, mfumo wetu wa hadhi na zawadi kwa wateja, ulioundwa kukupa zaidi kadri unavyoendelea kukua. Matumizi yako ya kila siku ya huduma za kifedha yanaweza kukupandisha kupitia viwango tofauti vya wateja, na kufungua manufaa maalum kila hatua unayofikia.
Bronze
Safari yako inaanzia hapa.
Silver
Punguzo la 5% kwenye GePG. Kikomo cha hadi USD 2,000.
Ruby
Punguzo la 10% kwenye GePG. Kikomo cha hadi USD 3,000.
Gold
Punguzo la 15% kwenye GePG. Riba ya hadi 8.5% kwenye Kibubu Fixed. Kikomo cha USD 5,000.
Platinum
Inakuja karibuni
Tanzanite
Inakuja karibuni
Alika marafiki tukulipe!
Marafiki zako wanastahili zaidi. Na wewe pia.
Mwalike rafiki ajiunge na Selcom Pesa na aanze kufanya miamala. Utapata bonasi yenye thamani ya 50% ya kifurushi atakachochagua, huku yeye akipata cashback ya 50% ya kifurushi alichojiunga nacho. Kadri unavyowaalika watu wengi zaidi, ndivyo unavyoweza kupata zaidi.
01 Alika
Waambie wapakue app ya Selcom Pesa na waweke namba yako ya simu ya Selcom Pesa kama referral code katika hatua ya mwisho ya usajili.
02 Wajiunge
Rafiki yako anajisajili na kuanza kutumia Selcom Pesa.
03 Wajiunge na bando
Rafiki yako anajiunga na kifurushi cha miamala kinachostahili, iwe ni kifurushi cha siku, wiki au mwezi.
04 Unapata bonasi
Unapata bonasi yenye thamani ya 50% ya thamani ya kila kifurushi, kwa kuzingatia masharti yanayotumika.
Selcom Pesa Mastercard. Pesa yako. Kwa mtindo wako.
Kadi yako ya kila siku ya debit, ya plastiki au kidijitali, iliyounganishwa moja kwa moja na akaunti yako ya Selcom Pesa. Fanya malipo mtandaoni, lipa kupitia POS, toa pesa kwenye ATM, na tumia Mastercard kufanya miamala ndani na nje ya Tanzania.
Ara Prepaid Card. Udhibiti zaidi.
Kutana na Ara Prepaid Card, kadi ya prepaid ya plastiki au kidijitali iliyoundwa kukupa njia nyingine rahisi ya kufikia na kutumia pesa zako. Weka pesa kwenye kadi yako. Itumie unapohitaji. Endelea kudhibiti matumizi yako.
Usalama wa kibenki
Usalama ni kipaumbele
Selcom Pesa inaweka usalama wa taarifa zako binafsi na za kifedha kuwa kipaumbele. App yetu imejengwa kwenye miundombinu salama yenye teknolojia ya hali ya juu ya usimbaji wa taarifa (encryption) na firewalls imara ili kulinda dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa. Kila muamala husimbwa kwa njia salama ili kuhakikisha taarifa zako zinaendelea kuwa siri. Ukiwa na Selcom Pesa, unaweza kusimamia fedha zako kwa kujiamini, ukijua kwamba taarifa zako zinalindwa.
Taarifa papo hapo
Fuatilia kila muamala wako kwa arifa za papo kwa papo kupitia app na SMS.
Kuingia kwa Usalama kwa Biometria
Fikia akaunti yako ya Selcom Pesa kwa haraka na kwa usalama ukitumia alama ya kidole au utambuzi wa uso, na kuongeza ulinzi wa ziada kwenye akaunti yako.
Usimamizi wa Kadi Ndani ya App
Angalia taarifa za kadi yako, fuatilia matumizi na endelea kuwa na udhibiti wa kadi yako popote ulipo.
Imeundwa kwa kuzingatia maisha halisi
Selcom Pesa inaendana na jinsi unavyoishi
Siku ya Mshahara Pokea pesa zako.
Kila Siku Lipa. Tuma. Nunua.
Siku ya Kuweka Akiba Weka pesa kwenye Kibubu.
Siku ya Safari Tumia Selcom Pesa Mastercard.
Siku ya Familia Tuma pesa kuvuka mipaka.
Siku Yoyote Mwalike rafiki na upate bonasi ya rufaa.