Selcom Yandaaa Futari Maalum kwa Watoto Yatima na Wanaoishi Katika Mazingira Magumu Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani

Katika kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Selcom team ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Ya Selcom Microfinance, Bw Julias Ruwaichi ilipata fursa ya kuandaa futari maalum kwa ajili ya watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto, vikiwemo Malaika Orphanage, Yoko Orphanage, Amani Children's Home, na Chakuama Orphanage.

Hafla hii iliwakutanisha watoto hawa katika kushiriki chakula cha jioni kwa pamoja, ikilenga kuleta faraja, mshikamano, na upendo miongoni mwao. Lengo kuu la iftari hii ni kuwaunganisha watoto wenye uhitaji, kuwapa nafasi ya kufurahia futari ya pamoja, huku ikihamasisha moyo wa kusaidiana na kutenda mema kama sehemu ya kumcha Mungu.

Selcom inaungana na Waislamu wote katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, tukithamini thamani ya mshikamano na upendo kwa wote.

Previous
Previous

Selcom Pesa Adds Color to the Color Festival 2025

Next
Next

Selcom Pesa Yashirikiana na Showmax kuwezesha Malipo bila makato kupitia kadi ya kidijitali Ya Selcom Pesa.