Unaendesha Biashara? Pokea Malipo kwa Urahisi na Selcom Lipa
Pokea Malipo kwa Urahisi na Selcom Lipa
Selcom Lipa (TANQR)
Kama mmiliki wa biashara, unastahili suluhisho la malipo linaloendana na mahitaji ya biashara yako. Kupitia Selcom Lipa (TANQR), unaweza kupokea malipo kwa haraka, kwa urahisi, na kwa njia zote, iwe ni kutoka kwa wateja wa mitandaoni au dukani.
Uhakiki wa TIN
Ukiwa na namba yako ya TIN na tarehe ya TIN pekee, unaweza kujisajili mara moja kupitia aplikesheni ya Selcom Pesa na kuanza kupokea malipo kutoka mitandao yote ya simu na benki zote, hivyo wateja wako wanaweza kukulipa kwa njia yoyote wanayopenda
Lipa Namba Moja – Popote Biashara Yako Ilipo
Haijalishi biashara yako iko wapi iwe ni dukani, mitandaoni (Facebook, Instagram, WhatsApp, TikTok), au hata tovuti yako unaweza kupokea malipo kwa urahisi kupitia Selcom Lipa. Unachohitaji kufanya ni kutuma Lipa Namba yako, na wateja wako wanaweza kukulipa papo hapo, bila kujali wamekupata wapi. Popote biashara yako ilipo, malipo yanafanyika kwa haraka bila usumbufu.
Jinsi Ya Kujisajili Kupata Selcom Lipa (TANQR)
Kwanini Uchague Selcom Lipa kutoka Selcom pesa?.
Selcom Lipa ni suluhisho la malipo lililoletwa kwa kuzingatia mahitaji ya wafanyabiashara wa aina zote.
Kupitia aplikesheni ya Selcom Pesa, unaweza kupokea malipo bila gharama yoyote ni huduma ya bure, rahisi kutumia, na yenye ufanisi mkubwa.
Malipo huingia moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Selcom Pesa, bila ucheleweshaji wala hatua za ziada.
Hakuna kikomo cha fedha unazoweza kupokea biashara yako ina nafasi ya kukua bila mipaka.
Haijalishi ukubwa wa biashara yako iwe biashara ndogo,biashara kubwa au ya mtandaoni. Unaweza kupokea malipo kupitia selcom lipa kwa wateja wako wote