5 kwa Jero

Fanya miamala 5 ya Lipa na/au Tuma Pesa kwa Shilingi 500 tu kiwango chochote kwa siku! Jiunge na Selcom Pesa sasa ufurahie Makato Madogo Kuliko!

Angalia video kujua jinsi ya kutumia ofa hii.

Je unajua ni kiasi gani cha makato unaweza kuokoa ukiwa na Selcom Pesa?

Tuma taarifa zako za miamala kwa kufuata hatua zifuatazo:

1. Nenda kwenye aplikesheni au USSD ya mtandao wako wa simu

2. Chagua Taarifa za Miamala

3. Chagua Tuma kwa barua pepe katika format ya PDF

4. Weka ujanja@selcompesa.app kama barua pepe itakayopokea taarifa moja kwa moja au pakua taarifa na tuma kwenda ujanja@selcompesa.app

5. Utapokea SMS yenye majibu ya kiasi cha makato ambacho ungeokoa ukiwa na Selcom Pesa ndani ya dakika 5.

Kwa kutuma taarifa za miamala, unakubaliana na masharti na vigezo hivi.

Uchambuzi umeongozwa na Tausi Africa (Manka).

Okoa Pesa ukiwa na Selcom Pesa - Inakupa Uhuru wa kutuma pesa, kufanya malipo kwa makato madogo kuliko na kusimamia fedha zako popote ulipo.

Tumefanya miamamala kuwa nafuu zaidi, kufika haraka, salama na yenye faida zaidi kwa kila Mtanzania ikiwemo Mfanyakazi, Mfanyabiashara, Mkulima, Mwanachuo, Gen Z au Alpha, Selcom Pesa ni kwa ajili yako!

Jionee Utofauti wa Makato na Selcom Pesa App

Makato madogo kuliko wote, mkeka mmoja miamala mbalimbali. Tuma pesa kutoka Selcom Pesa kwenda mitandao ya simu, benki zote na kulipia bili mbalimbali kwa Lipa namba.

Kutuma pesa kutoka Selcom Pesa kwenda Selcom Pesa, Hakuna Makato!

Tuma kwa Yeyote, Tuma kwa Wengi

Kupitia Selcom Pesa unaweza kutuma pesa kwenda benki yoyote, mitandao yote ya simu, kutuma kwa wanufaika zaidi ya mmoja kwa mara moja huku ukifuruhia makato madogo kuliko wote.

Tuma Pesa kwenda benki na mitandao yote.

“Tuma kwa Wengi” hukuwezesha kufanya malipo kwa walengwa wengi kwa wakati mmoja!

Weka pesa uanze kufanya miamala yenye makato madogo zaidi ukiwa na Selcom Pesa App. Weka kwa urahisi kupitia mitandao ya simu, benki na wakala wa Selcom.

  • Kutumia USSD au Aplikesheni:

    1. Nenda kwenye sehemu ya Tuma Pesa kwenda Benki.

    2. Chagua benki - Selcom Microfinance Bank (zamani Access Microfinance Bank).

    3. Weka namba ya akaunti ya Selcom Pesa au namba ya simu uliyojisajili na Selcom Pesa App.

    4. Weka kiasi cha kutuma.

    5. Ingiza PIN ili kuthibitisha.

  • Kutumia USSD au Aplikesheni ya Benki:

    1. Nenda kwenye sehemu ya Tuma Pesa kwenda Benki.

    2. Chagua benki - Selcom Microfinance Bank (zamani Access Microfinance Bank).

    3. Ingiza namba ya akaunti ya Selcom Pesa au namba ya simu uliyojisajili na Selcom Pesa App.

    4. Weka kiasi.

    5. Ingiza PIN ili kuthibitisha.

  • 1. Tembelea wakala wa Selcom Huduma aliye karibu nawe

    2. Toa pesa taslimu

    3. Toa akaunti yako ya Selcom Pesa App au namba ya simu uliyojisajili na Selcom Pesa App au namba ya kadi

    4. Pokea SMS ya uthibitisho

  • Weka namba ya akaunti au namba ya simu uliyojisajili na Selcom Pesa App, jina, sarafu, na SWIFT code ya Selcom Microfinance Bank (ambayo ni ACTZTZTZ)

Kufanya Miamala ni Simpo tu!

Lipia bidhaa na huduma kwa mfanyabiashara yeyote Tanzania kwa kutumia TanQR/Namba ya Lipa ya Selcom au Lipa namba ya mitandao ya simu yote au Lipa namba ya benki zote kwa makato yaleyale ambayo ni madogo na nafuu zaidi.

Lipa kwa Simu. Mlipe mtoa huduma kwa Lipa Namba au QR Code

Bili mbalimbali na malipo ya Serikali. Hakuna foleni, hakuna kuhangaika!

Jisevie na Kibubu

Tunza pesa zako na Kibubu kwa kuweka asilimia ya kila muamala au kiasi maalum utakacho. Akiba ya Kibubu inaweza kuwa ya kuingiza kiasi au ya kukokotolewa kiotomatiki kutoka kwenye miamala. Kumbuka haba na haba hujaza kibubu.

Timiza malengo ukiwa na Kibubu—weka malengo, fuatilia na tazama ndoto yako ikitimia!

Miamala Yenye Zawadi

Jipatie Qwikrewards kupitia miamala na ofa maalum za mara kwa mara. Unaweza kutumia Qwikrewards zako kukamilisha malipo ya wafanyabiashara au bili mbalimbali.

Qwikrewards ni programu ya zawadi kwa wateja waaminifu inayopatikana kupitia kupitia USSD na aplikesheni. Programu hii inawawezesha makampuni kutoa zawadi, pointi au marejesho ya fedha kwa wateja wao wanaochagua kufanya miamala kidijitali. Qwikrewards inaletwa kwako na Selcom.

Jipatie Selcom Pesa Mastercard

Pata kadi yako kwa urahisi na haraka. Unganisha na aplikesheni ya Selcom Pesa na kuanza matumizi papo hapo. Pia unaweza kuunda kadi ya kidijitali ili kufanya malipo ya mtandaoni na zaidi bila makato. Dhibiti matumizi ya kadi moja kwa moja ukiwa ndani ya aplikesheni.

Jinsi ya Kuunganisha Selcom Pesa Mastercard kwenye Selcom Pesa App. 

Selcom Pesa Mastercard ni kadi ya benki inayounganishwa moja kwa moja kwenye Selcom Pesa App yako. Unaweza kuitumia kutoa pesa kwenye ATM yoyote yenye nembo ya Mastercard na kufanya malipo ya BURE mtandaoni na kwenye mashine za mauzo (POS).

Fuata hatua hizi rahisi kuunganisha Selcom Pesa Mastercard yako na Selcom Pesa App yako

  • Tembelea tawi lolote la Selcom Microfinance Bank lililopo Temeke, Lumumba, au Kijitonyama au fika kwenye Xperience Centres zetu zilizopo Barabara ya Haile Selassie au Kariakoo (mtaa wa Uhuru na Nyamwezi). Timu yetu ya huduma kwa wateja itakukabidhi Selcom Pesa Mastercard yako.

      1. Fungua Selcom Pesa App na nenda kwenye sehemu ya Akaunti Yangu.

      2. Vuta chini kadi ya kwanza inayojitokeza juu ya skrini.

      3. Bonyeza kitufe cha "Unganisha Kadi."

      4. Weka namba ya kadi iliyopo juu ya msimbo/QR nyuma ya kadi yako au skani msimbo/QR.

      5. Ingiza CVV (namba tatu zilizopo nyuma ya kadi yako) na bonyeza Endelea.

      6. Tengeneza PIN ya kadi yako na thibitisha kwa kugusa Unganisha Kadi.

      7. Uthibitisho utatumwa kupitia SMS. TZS 2,500 itakatwa kutoka kwenye akaunti yako kama ada ya kadi.

  • Selcom Pesa Mastercard yako sasa imeunganishwa kikamilifu na Selcom Pesa App yako. 

    Anza kufurahia miamala rahisi, malipo ya bure mtandaoni na kwenye POS, pamoja na kutoa pesa kwa usalama kwenye ATM yoyote yenye nembo ya Mastercard.

Matumizi Ndio Mpango Mzima

Fuatilia matumizi yako mubashara kupitia grafu ya matumizi ya kila mwezi. Tumekurahisishia ufuatatiliaji wa matumizi yako.

Usalama wa Uhakika

Jiamini ukiwa na Selcom Pesa. Taarifa zako na za miamala yako zipo salama. Tunakuhakikishia ulinzi imara.

Taarifa za papo hapo.

Fuatilia miamala yako inayoingia na kutoka moja kwa moja ndani ya aplikesheni na SMS.

Usalama. Ingia kwa kuskani.

Kukuhakishia usalama zaidi tumekuwezesha kuingia kwenye aplikesheni kwa kutumia utambulisho wa kibayometriki wa uso, kidole au namba ya siri.

Dhibiti matumizi ya kadi.

Je kadi yako imeibiwa au imepotea? Unaweza kuifunga au kuisitisha ukiwa ndani ya aplikesheni

Fungua Akaunti Kijanja

Jisajili mwenyewe na fungua akaunti kwa kutumia namba yako ya simu, kitambulisho cha NIDA na taarifa za kibayometriki za vidole na uso ndani ya DAKIKA CHACHE!

Tutumie Ujumbe